Friday, January 4, 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE AUNGANA NA MAELFU YA WAOMBOLEZAJI KUMZIKA MAREHEMU JUMA KILOWOKO 'SAJUKI' JIJINI DAR

Maelfu waliojitokeza kumzika marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki' katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wasanii wakijipanga kumzika marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki'.
 Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki' likiwasili makaburini tayari kwa maziko.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Jakaya Kikwete akiwa ni mmoja ya waombolezaji waliojitokeza katika maziko ya msanii huyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Jakaya Kikwete akiweka udongo kwenye Kaburi la Marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki' yaliyofanyika mchana huu kwenye Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam.
 Mawasiliano ya hapa na pale.
 Waombolezaji waliojotokeza katika maziko ya Msanii Sajuki wakiwa katika utulivu.
 Mh. Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa akidiliana jambo na wasanii.
 Wasanii wakijipanga kupokea wageni.
 Mbunge wa Kigoma Mh. Zitto Kabwe alikuwa ni miongoni wa waombolezaji waliojitokeza kumzika Marehemu Sajuki.
 Waombolezaji wakiwa wamejipanga kupokea jeneza la Marehemu Sajuki.
 Jeneza lililobeba mwili wa  marehemu Sajuki likiingizwa  makaburini.
 Mchezaji wa Simba, Juma Kaseja akiingia makaburini pamoja na mtangazaji wa Clouds Fm, Bwinga (kwanza kulia).
 Ilikuwa ni mshike mshike kwa waandishi kila mmoja akitaka kupata picha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete akiwa na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania,Saimon Mwakifwamba pamoja na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa wakati wa maziko ya marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki'.
 Waombolezaji wakiweka udongo katika kaburi la Marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki'
 
Maelfu ya waombolezaji waliojitokeza kumzika marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki' leo katika makabiri ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI!

MATUKIO KATIKA MSIBA WA MAREHEMU SAJUKI JIJINI DAR


Mkurugenzi wa Maendeleo na Utamaduni wa Wizara ya Habari Bw. Herman Mwasoka (mwenye suti nyeusi) akimfariji Baba mzazi wa Marehemu Sajuki Mzee Juma Kilowoko alipofika nyumbani kwa marehemu kuhani msiba huo Tabata Bima jijini Dar. (Picha zote na Mo Blog).
Mkurugenzi wa Utamaduni na Maendeleo wa Wizara ya Habari Bw. Herman Mwasoka akitia saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Sajuki jijini Dar leo.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bi. Joyce Fisso akitia saini kitabu cha maombolezo ya Msiba wa Sajuki.
Msanii mkongwe katika tasnia ya muziki wa Dansi na Rhumba Kikumba Mwanza Mpango almaarufu kama King Kiki akitia saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Marehemu Sajuki Tabata Bima jijini Dar leo.
Mzee King Kiki akiteta jambo na Mkurugenzi wa Utamaduni na Maendeleo wa Wizara ya Habari Bw. Herman Mwasoka (katikati) nyumbani kwa marehemu Sajuki jijini Dar leo. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bi. Joyce Fisso
Wasanii mbalimbali na wakiendelea kuwasili nyumbani kwa Marehemu Sajuki Tabata Bima jijini Dar es Salaam. Pichani ni Msanii wa muziki Dokii (kushoto) sambamba na Mshiriki wa Shindano la Big Brother Africa Mwisho Mwampamba na wasanii wengine.
Mchekeshaji maarufu wa The comedy Masanja Mkandamizi akijifuta jasho kwa mbali akielekea msibani nyumbani kwa Marehemu Sajuki. Masanja alikuwa ni mmoja wa wahamishaji katika kuchangia pesa za matibabu ya marehemu Sajuki kwenda nchini India kupitia kipindi cha Luninga cha The Comedy kinachorushwa na Televisheni ya TBC.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa kwenye huzuni kutafakari kifo cha Sajuki.
VIONGOZI WA SERIKALI WAKIWASILI: Mbunge wa jimbo la Segerea, Dar es Salaam, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (wa tatu kushoto) akiwa ameambatana na Mbunge wa jimbo la Kinondoni Mh.Iddi Azzan wakipokelewa na Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Bw. Simon Mwakifamba na wasanii wengine wa filamu baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Sajuki kwa ajili ya kuhani msiba huo.
Mkuu wa Itifaki Bw. Simon Simalenga wa Clouds Media akimuongoza Mh.Makongoro Mahanga sehemu maalum kwa ajili ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
Mbunge wa jimbo la Segerea, Dar es Salaam, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akitia saini katika kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Sajuki.
Mbunge wa Kinondoni Mh. Iddi Azzan naye aliangusha saini kwenye kitabu hicho.
Mzee King Kiki  akizungumza jambo na Waheshimiwa Wabunge kwenye msiba wa Sajuki Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.
Waheshimiwa wakielekea nyumba ya jirani walikokusanyika baadhi ya waombolezaji na wasanii wa filamu nchini kwa ajili ya kuzungumza machache na kutoa Ubani.
Katibu wa Fedha msibani hapo mchekeshaji maarufu Steve Nyerere akiwakaribisha waheshimiwa wabunge kuzungumza na hadhira ya waombolezaji (hawapo pichani).
Mbunge wa jimbo la Segerea, Dar es Salaam, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akitoa salamu zake za rambimbi na kuahidi kuchangia shilingi 200,000/= kwa ajili ya kufanikisha shughuli za mazishi ya mpendwa wetu Marehemu Sajuki atakayezikwa Kesho Ijumaa katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Mh. Iddi Azzani akielezea kwa majonzi alivyopokea taarifa za msiba wa Sajuki na kuahidi kushirikiana bega kwa bega na Wastara panapomajaliwa ya Mola katika malezi ya mtoto aliyeachwa na marehemu na kuwaasa wadau, ndugu, jamaa na marafiki kumsaidia Wastara kutokana na hali yake na amechangia kiasi cha Shilingi 500,000= kufanikisha shughuli za mazishi ya marehemu Sajuki.
Pichani Juu na Chini ni Umati wa waombolezaji ukisikiliza nasaha za waheshimiwa Wabunge (hawapo pichani) walipofika nyumbani kwa marehemu Sajuki kuhani msiba huo.
Kazi ya kuosha vyombo si kina Dada tu, hata kina Kaka wanaweza pia....Pichani ni baadhi ya Watangazaji wa Clouds Radio wakiongozwa na Dina Marios kushiriki kuosha vyombo vilivyotumika katika msiba huo huku wakisaidiana na waombolezaji wengine.
Mganga wa Jadi anayefahamika kwa jina la Dokta Manyaunyau (kushoto) sambamba na Msanii wa filamu nchini Cloud wakisikiliza mawaidha ya waheshimiwa wabunge (hawapo pichani).
Mkuu wa Itifaki msibani hapo Bw. Simon Simalenga wa Clouds Media akimpokea Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete alipowasili nyumbani kwa marehemu Sajuki kwa ajili ya kuhani maeneo ya Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete akitoa pole baada ya kusaili kwa baadhi ya ndugu wa karibu wa marehemu Sajuki msibani hapo.
  Bw.Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Baba mzazi wa marehemu Sajuki Mzee Juma Kilowoko nyumbani kwa marehemu Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Sajuki leo.
  Bw.Ridhiwani Kikwete akimpa maneno ya faraja Baba mzazi wa Marehemu Sajuki Mzee Juma Kilowoko.
  Bw.Ridhiwani Kikwete akitoa mkono wa pole kwa mke wa marehemu Sajuki Bi. Wastara (mwenye buibui).
  Bw.Ridhiwani Kikwete akimfariji mama mzazi wa Marehemu Sajuki alipofika nyumbani hapo kuhani msiba huo.
Katibu wa fedha msibani hapo Steve Nyerere akitetea jambo na Bw. Ridhiwani Kikwete.
 Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Bw. Simon Mwakifamba akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Bw. Ridhiwani Kikwete kuzungumza machache na waombolezaji.
Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete akizungumzia marehemu Sajuki na kuwataka wanawake kuiga mfano wa Maisha ya Sajuki na Wastara jinsi walivyokuwa wakiishi na Upendo mpaka Umauti ulipomkuta marehemu Sajuki na kuwasisitiza kuenzi yale yote mema aliyokuwa akifanya kipindi cha uhai wake na kuwamasisha Umoja na Mshikamano baina yao. Bw. Ridhiwani Kikwete naye alichangia Shilingi 500,000/= kwa ajili ya kufanikisha mazishi ya Mpendwa wetu Sajuki anayetarajiwa kuzikwa Kesho Ijumaa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya wasanii wa filamu wakisikiliza nasaha za Bw. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani).
Marehemu Sajuki alikuwa kipenzi cha watoto na wakubwa pia. Pichani ni Umati wa watoto wanaokaa jirani na Nyumba ya Marehemu Sajuki wakiwa wamekusanyika huku wakionyesha majonzi na simanzi tele.