Tuesday, October 30, 2012

KAMA HUKUONA BEHIND THE SCENES YA TANGAZO LA EBSS, NATABIRI SALMA YUSUPH KUONDOKA NA 50MILLION CASH PRIZE


 Hiyo ni behind the scene ya Tangazo la Epiq Bongo Star Search 2012
Natabiri tu jamani, kwa ufuatiliaji wangu wa Epiq Bongo Star Search 2012 naona kabisa huyu Salma Yusuf anaujua anafanya nini. Nampenda sana tangu nimuone siku ya kwanza kwenye audition za Zanzibar pale ngome kongwe. Ili kuufanya utabiri wangu utimie TUMA NENO 'EBSS09 KWENDA 15503

Monday, October 29, 2012

OFFICIAL TRAILER YA KUM KUBUM YA NIKKI WA PILI,ICHEKI HAPO CHINI

UTENGENEZAJI WA COVER YA TRACK MPYA YA DIAMOND IITWAYO "NATAKA KULEWA"

Huyo jamaa mweupe anaitwa Zungu, yuko na jamaa location wakijiandaa kushoot picha za cover hiyo.
.
.
.
.
.
 
 Raqey akiwa kwenye kazi yake kama kawaida. Huyu jamaa ni mzuri sana kwenye hayo mambo.
.
Jinsi Cover lilivyotokelezea

.

Friday, October 19, 2012

KILINUKA SANA LEO DAR ES SALAAM, IPO HAJA KUBWA YA KUTAFUTA UFUMBUZI WA HARAKA!

 
Wananchi wakitawanyika wakati wa vurugu eneo la Msimbazi, Kariakoo jijini Dar.
 
Polisi wakiimarisha ulinzi eneo la Kariakoo leo.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa leo katika maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam baada ya polisi kuzuia maandamano yaliyotaka kufanywa na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kitendo kilichopelekea mabomu ya machozi kulipuliwa na baadhi ya waumini hao kutia nguvuni na polisi.
 
Magari ya Jeshi la Wananchi Tanzania yakielekea Kariakoo kwa ajili ya kuimarisha ulinzi eneo hilo.
 
Jamaa huyu alidakwa na polisi wakati wa maandamano hayo.
 
Polisi wakiwatangazia wananchi waliokuwa eneo la Kariakoo kutawanyika mara moja wakati wa vurugu hizo.
 
Mama huyu alipoteza fahamu baada ya milipuko kadhaa kutokea eneo hilo.
 
Polisi wakiwa kazini kuzuia maandamano hayo.
 
Baadhi ya waandamanaji waliokamatwa wakati wa vurugu hizo wakiingizwa kituo cha polisi Msimbazi.

 
Magari ya Jeshi la Wananchi yakipita katika mitaa ya Kariakoo kuwataarifu wananchi kutawanyika eneo hilo.
Baada ya baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kutawanywa kwa mabomu na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia hapo awali, kwa sasa waumini hao wanajipanga kuvamia kituo cha polisi mtaa wa Msimbazi wakiwa katika makundi makundi mikononi wakiwa na mawe na wakiimba nyimbo. Awali magari ya Jeshi la Wananchi yalipita mitaa ya Kariakoo yakiwa na wanajeshi waliokuwa wakiamuru wananchi kutawanyika lakini hali inaonekana kubadilika maana kwa sasa waumini hao wanajikusanya upya kutimiza azma yao ya kuandamana mara baada ya kumaliza swala ya saa 10 katika msikiti wa Idrissa uliopo Kariakoo. Baadhi ya madai ya waumini hao ni KUKAMATWA SHEIKH PONDA, KUTOONEKANA KWA SHEIKH FARIDI WA ZANZIBAR NA KUKOJELEWA QURAN.

Friday, October 12, 2012

"BREAKING NEWS" VURUGU ZATOKEA MBAGALA KIZUIANI DAR ES SALAAM

Habari nilizozipata hivi punde zinadai vurugu kali zatokea eneo la mbagala kizuiani jijini Dar es Salaam baada ya Waislamu wenye hasira kali kutaka kuvamia na kukichoma moto kituo cha polisi katika eneo hilo endapo wasipopatiwa kijana aliedaiwa kukikojolea kitabu cha Quran takatifu. Tukio hilo la aina yake lililofanywa na kijana mdogo anaedaiwa kuwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza lilitokea baada ya mabishano kati yake na mwenzake ambapo walibashana kuwa mtu akikojolea kitabu hicho kitakatifu atapata uchizi, hatimaye dogo huyo akaamua kukiojolea kitabu hicho ili kumpinga rafiki yake huyo ambae nae sina taarifa zake za uhakika. Nitaendelea kukujuza zaidi kadiri habari zitakavyonifikia. Ushahidi wa picha hizo hapo chini kwa hisani ya GPL.






KINGINE KIZURI KUTOKA SETH BOSCO'S BLOG NA KANUMBA THE GREAT FILMS COMPANY.

Blog hii inakupatia nafasi wewe msomaji mjasiriamali ya kujitangaza na kutangaza biashara yako au huduma mbalimbali kama vile Catering Services, Nyumba zinazouzwa, magari, viwanja, pamoja na biashara za makampuni mbalimbali. Tangazo lako litapata nafasi ya kusomwa na zaidi ya watu elfu tano kila wiki wanaotembelea blog hii. Fursa hii ni kwa wafanyabiashara wa ngazi zote na kada tofauti. Pia tunatoa taarifa za vifo,harusi,sherehe mbalimbali pamoja na kupotelewa na vitu au mtu. Bei zetu ni sawa na bure, wasiliana nasi kwa E-Mail: seththepioneer@gmail.com au tupigie kwa +255715809043

"Lets STAND for Africa" Steven Kanumba

Wakati shirika la chakula duniani mapema jana lilitoa takwimu zilizoonesha kuwa bara la Afrika linafanya vizuri kupigana na njaa pamoja na upungufu wa chakula likiwa mbele ya mataifa ya bara la Asia kama India na mengineyo video hiyo hapo chini ulikua ujumbe kwa Wafrika wote uliotolewa na Steven Kanumba akisisitiza waafrika kulitetea bara lao na kulisimamia katika masuala mbalimbali ikiwemo usalama wa chakula pamoja na amani.

KAMA HUKUONA MKASI NA RAY KIGOSI ITAZAME HAPA ALIFUNGUKA PIA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA MAREHEM KANUMBA!

Wednesday, October 10, 2012

MAN OF THE PEOPLE







PICHA KATIKA MATUKIO  MBALIMBALI YA KIJAMII AMBAYO STEVEN ALIJIHUSISHA. HAPA ALIKUA KATIKA KAMPENI YA MAMA SHUJAA WA CHAKULA YA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA OXFAM AMBAPO YEYE ALIKUA BALOZI WAKE.

Monday, October 1, 2012

IPO SIKU MTALIPWA KAMA MNAVYOLIPWA KWA KUSEMA UONGO

KAMA HUKUONA HII NDIO ILIKUA CHRISTMASS YA MWISHO KWA KANUMBA

THE GREAT NA X MASS...

Mara baada ya kutoka kanisani niliandaa chakula nyumbani kwangu,nikachoma nyama ya mbuzi na kuku,nikaandaa vinywaji,basi nikawaarika ndugu na jamaa wachache tu waje nyumbani tufurahi xmass hii.Kila mtu nilihakikisha anapata kinywaji anachopenda hata wanywaji wa pombe nao walipata wanachokipenda.Maandiko yanasema tazama ilivyo vyema kwa ndugu kukaa pamoja na kufurahi.
Sebuleni kwangu ndio kulikuwa counter...ahhahah
Walikuepo wazee wa konyagi,wazee wa nyama choma ahahahh
Story za hapa na pale zilikuepo.
Kubadilishana mawazo.
The great na bbm?kha?

Watu wakafurahi nami nikafurahi maana nimekuwa busy sana mara shooting,mara safari nje ya nchi,mara safari za Startimes,mara safari za Oxfam,mara busy ofisini nakosa mda wa kujumuika hivi nyumbani,hivyo x mass hii nikaimaliza hivi.Zaidi ya yote sifa na utukufu nikamrudishia GEHOVA EBENEZER,GEHOVA ELISHADAI,GEHOVA SHAMA.......EMMANUEL(Mungu pamoja nasi)>>>>Originally posted by Steven Kanumba HAPA on December 26,2011<<<<<<<

Hivyo ndivyo ilivyosomeka katika blog yake siku ya tarehe 26 Desemba mwaka 2011. Napenda niseme tu kuwa siku zote ambazo nimeishi na kaka yangu marehemu Kanumba sikuwahi kufikiria kama ipo siku atakuja kuondoka kama alivyoondoka,tuliishi kwa furaha,amani upendo na ushirikiano wa hali ya juu sana,sikuonekana katika picha hizo ila nilikuepo na ndie niliepiga picha hizo. Najaribu tu kuwaonesha maisha yangu na Kanumba siku za karibia na kifo chake ili mpate kujua msichokua mnakifahamu. Mungu ailaaze roho yake mahala pema peponi.

HII INAKUHUSU SANA,NI MANENO YA STEVEN KANUMBA KTK BLOG YAKE ENZI ZA UHAI WAKE!

MANENO YANGU KWA MASHABIKI WANGU WOTE WANAOPITIA AU WALIOPITIA MAISHA MAGUMU KTK FAMILIA(,DIFFERENT SEASONS&FLAVOURS) .

THE FOLLOWING PICTURES ARE OF THE SAME BUT TAKEN AT DIFFERENT SEASONS..STAY BLESSED AND ENJOY THE SEASONS OF YOUR LIFE.



LESSONS ON LIFE:=U can not judge a tree or a person by only one season,and that the essence of who they are and the pleasure,joy and love that come from that life can only be measured at the end when all the seasons are up.If you give up when its winter u will miss the promise of your spring,the beauty of your summer and the fulfillment of your fall......MORAL:=Don't let the pain of one season destroy the joy of all the rest.Don't judge life by one difficult season.Thank u...Steve Kanumba.(Originally posted by Steven Kanumba on Feb 9,2012)