Polisi wakiimarisha ulinzi eneo la Kariakoo leo.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa leo
katika maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam baada ya polisi kuzuia
maandamano yaliyotaka kufanywa na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu
kitendo kilichopelekea mabomu ya machozi kulipuliwa na baadhi ya waumini
hao kutia nguvuni na polisi.
Magari ya Jeshi la Wananchi Tanzania yakielekea Kariakoo kwa ajili ya kuimarisha ulinzi eneo hilo.
Jamaa huyu alidakwa na polisi wakati wa maandamano hayo.
Polisi wakiwatangazia wananchi waliokuwa eneo la Kariakoo kutawanyika mara moja wakati wa vurugu hizo.
Mama huyu alipoteza fahamu baada ya milipuko kadhaa kutokea eneo hilo.
Polisi wakiwa kazini kuzuia maandamano hayo.
Baadhi ya waandamanaji waliokamatwa wakati wa vurugu hizo wakiingizwa kituo cha polisi Msimbazi.
Magari ya Jeshi la Wananchi yakipita katika mitaa ya Kariakoo kuwataarifu wananchi kutawanyika eneo hilo.
Baada ya baadhi ya waumini wa
dini ya Kiislamu kutawanywa kwa mabomu na askari wa Kikosi cha Kutuliza
Ghasia hapo awali, kwa sasa waumini hao wanajipanga kuvamia kituo cha
polisi mtaa wa Msimbazi wakiwa katika makundi makundi mikononi wakiwa na
mawe na wakiimba nyimbo. Awali magari ya Jeshi la Wananchi yalipita
mitaa ya Kariakoo yakiwa na wanajeshi waliokuwa wakiamuru wananchi
kutawanyika lakini hali inaonekana kubadilika maana kwa sasa waumini hao
wanajikusanya upya kutimiza azma yao ya kuandamana mara baada ya
kumaliza swala ya saa 10 katika msikiti wa Idrissa uliopo Kariakoo.
Baadhi ya madai ya waumini hao ni KUKAMATWA SHEIKH PONDA, KUTOONEKANA
KWA SHEIKH FARIDI WA ZANZIBAR NA KUKOJELEWA QURAN.
No comments:
Post a Comment