Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu
Dar es salaam jana december 21 2012 imefunga jalada la kesi ya kuua
bila kukusudia inayomkabili mwigizaji Elizabeth Michael maarufu kama
Lulu tayari kwa kulipeleka Mahakama kuu ya Tanzania ili hiyo kesi ianze
kusikilizwa.
Kabla ya kusomwa kwa maelezo ya
kesi hiyo ambapo Lulu hakutakiwa kujibu chochote kutokana na Mahakama
ya Kisutu kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, Hakimu wa
Mahakama ya Kisutu Augustina Mmbando amemtaka wakili wa serikali kutaja
idadi ya mashahidi watakaotoa ushahidi wao wakati kesi hiyo itakapoanza
kusikilizwa.
Wakisoma kwa awamu maelezo ya
mashahidi wa kesi hiyo, mawakili wa serikali kwenye hiyo kesi wamesema
wanao mashahidi tisa wanaotarajiwa kuwatumia kwenye kesi na kuongeza
kwamba shahidi namba moja ni Seth Bosco mdogo wa Marehemu Kanumba
waliekua wakiishi pamoja.
Kwenye maelezo yaliyosomwa na
Seth mahakamani, imeelezwa kwamba siku ya tukio Kanumba alimtaka asitoke
ili watoke pamoja baadae lakini ilipofika saa tano usiku alisikia
vurugu chumbani kwa Kanumba ambako alikua na mpenzi wake ambae ni Lulu
na baada ya muda Seth aligundua kulikua na ugomvi unaendelea na mlango
ulikua umefungwa.
Maelezo hayo yameendelea kwamba
baada ya muda Lulu alitoka chumbani kwa Kanumba na kumtaarifu Seth
kwamba Kanumba ameanguka ambapo Seth alipoingia chumbani alikuta Kanumba
kaegemea ukuta pembezoni mwa mlango huku povu likimtoka mdomoni na
kuamua kumlaza chini kabla ya kuomba msaada.
Mashahidi wengine wanaotarajiwa
kutoa ushahidi wao wakati kesi itakapoanza kusikilizwa ni Sophia Kassim
ambae ni mmiliki wa nyumba aliyokua anaishi Kanumba, madaktari watatu,
Polisi watatu, afisa uhamiaji ambae ni shemeji wake Kanumba na Moris
Sekwao ambae ni kijana aliempakia Lulu kwenye gari lake muda mfupi kabla
ya kukamatwa.
Baada ya kusomwa kwa maelezo ya
mashahidi wote, wakili wa serikali amesoma maelezo ya Lulu na kuamplfy
kwamba mwigizaji huyu alianza uhusiano wa kimapenzi na Kanumba january
2012 ambapo walikua na kutoelewana katika baadhi ya nyakati hasa pale
mmoja anapompigia simu mwenzake na haipokelewi kwa wakati.
Baada ya maelezo yote kutolewa
na kukamilika, Hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Augustina
Mmbando amezishukuru pande zote na kumtaka Lulu atoe maelezo ya nyongeza
kama anayo ambapo Lulu alisema hana maelezo yoyote ya kuongezea.
Hakimu Mmbando amemtaka Lulu kuendelea kubaki rumande mpaka tarehe ya kesi yake itakapotajwa na Mahakama kuu ya Tanzania.
Hakuna ukweli wowote wa taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Lulu ameachiwa kwa dhamana.
mi nashangaa hao waliozusha hivo hawawezi kumpa dhamana kirahisi hivyo watu si watamuua mtaani kwa usalama wake akae tu huko mpaka watu hasira zipungue
ReplyDeleteshukrani kwa update
ReplyDelete