Siku ya Jumapili tarehe 7 Aprili 2013 ilikua siku ya kumbukumbu ya kifo cha Steven Kanumba ambapo familia kwa kushikiana na wadau mbalimbali iliandaa ibada maalumu iliofanyika kanisa la KKKT Usharika wa Kimara Temboni, kisha kutembelea ikiwa ni pamoja na kuwasha mishumaa na kuweka mashada ya maua katika kaburi la marehemu. Na baada ya hapo majira ya saa mbili usiku kulikua na uzinduzi wa filamu ya mwisho ya Kanumba na Marehem Sharo Millionaire ilioambatana na filamu maalumu ilioandaliwa na msanii Jackline Wolper ikiwashirikisha wasanii waliowahi kufanya kazi na Marehemu Steven Kanumba. Pia familia ilitoa tuzo za shukran kwa makampuni na watu binafsi waliochangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha maisha ya Steven na hata baada ya kufariki waliendelea kutoa mchango huo ikiwa na pamoja na wanahabari kwa ujumla wao.
Staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, akiwa na shada la maua pembeni yake ni mama wa marehemu, Flora Mtegoa.
Mdogo wa marehemu Kanumba, Seth Bosco, akiwaongoza wasanii kutoka Ghana kuweka mashada ya maua juu ya kaburi la Kanumba.
Msanii Yusuf Mlela akiwa na simanzi kaburini kwa Kunumba.
Shabiki mmoja akilia kwa uchungu juu ya kaburi la Kanumba.
Wasanii mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja kwenye kaburi la Kanumba.
|
Millard Ayo wa Cloudsfm Amplifaya akipokea tuzo yake{Ikumbukwe kuwa Millard Ayo aliandaa short documentary nzuri sana ya maisha ya Steven Kanumba} |
|
Millard Ayo akitoa shukran kwa wasikilizaji wa kipindi chake cha Amplifaya |
|
Mwakilishi wa IPP Media akipokea tuzo yao |
|
Mtahiki Meya wa manispaa ya Kinondoni akipokea tuzo ya Rais Jakaya Kikwete |
|
Jacky Wolper |
|
MC Babu Ayubu |
|
Simon Mwakifwamba akipokea tuzo kwa niaba ya TAFF |
|
Zamaradi akipokea tuzo kwa niaba ya Clouds Media Group |
Mama Flora Mtegoa, Nana(Ghallywood), Mama Lema na Ama K(Ghallywood)
Picha zaidi zinakuja. Endelea kutembelea www.sethboscotz.blogspot.com