Monday, December 24, 2012

INAUMA SANA, NI KAMA NDOTO, HII NDIO ILIKUA XMASS YA MWISHO KWA KANUMBA

Ni kama ilikua jana nikiangalia picha hizi nakumbuka mengi yaliotokea siku hiyo hakuna alietarajia kuwa hatutakua na Kanumba x-mass hii. Tutakukumbuka daima kwa ucheshi, upendo, ukarimu na Mengi alikujalia Mwenyezi Mungu.

Kuanzia kushoto ni Issaya Kandonga 'IK', Shadyah IK, The Great, Fahim na Steven Nzelu
Kwa maneno yake aliandika hivi "Mara baada ya kutoka kanisani niliandaa chakula nyumbani kwangu,nikachoma nyama ya mbuzi na kuku,nikaandaa vinywaji,basi nikawaarika ndugu na jamaa wachache tu waje nyumbani tufurahi xmass hii.Kila mtu nilihakikisha anapata kinywaji anachopenda hata wanywaji wa pombe nao walipata wanachokipenda.Maandiko yanasema tazama ilivyo vyema kwa ndugu kukaa pamoja na kufurahi."
Kuanzia kushoto ni Qwihsar Thompson 'Q' wa CloudsTv, Friend, Edwin Kileo 76, Irene Paul na TheGreat

"Sebuleni kwangu ndio kulikuwa counter...ahhahah"
Walikuepo wazee wa konyagi,wazee wa nyama choma ahahahh
Story za hapa na pale zilikuepo.
Kubadilishana mawazo.
The great na bbm?kha?

Akamaliza kwa kusema "Watu wakafurahi nami nikafurahi maana nimekuwa busy sana mara shooting,mara safari nje ya nchi,mara safari za Startimes,mara safari za Oxfam,mara busy ofisini nakosa mda wa kujumuika hivi nyumbani,hivyo x mass hii nikaimaliza hivi.Zaidi ya yote sifa na utukufu nikamrudishia GEHOVA EBENEZER,GEHOVA ELISHADAI,GEHOVA SHAMA.......EMMANUEL(Mungu pamoja nasi)"

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI.

Saturday, December 22, 2012

WATANZANIA, MAELEZO YOTE KUHUSU KINACHOENDELEA KWENYE KESI YA MWIGIZAJI LULU YAKO HAPA!

 
Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam jana december 21 2012 imefunga jalada la kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili mwigizaji Elizabeth Michael maarufu kama Lulu tayari kwa kulipeleka Mahakama kuu ya Tanzania ili hiyo kesi ianze kusikilizwa.
Kabla ya kusomwa kwa maelezo ya kesi hiyo ambapo Lulu hakutakiwa kujibu chochote kutokana na Mahakama ya Kisutu kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, Hakimu wa Mahakama ya Kisutu Augustina Mmbando amemtaka wakili wa serikali kutaja idadi ya mashahidi watakaotoa ushahidi wao wakati kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa.
Wakisoma kwa awamu maelezo ya mashahidi wa kesi hiyo, mawakili wa serikali kwenye hiyo kesi wamesema wanao mashahidi tisa wanaotarajiwa kuwatumia kwenye kesi na kuongeza kwamba shahidi namba moja ni Seth Bosco mdogo wa Marehemu Kanumba waliekua wakiishi pamoja.
Kwenye maelezo yaliyosomwa na Seth mahakamani, imeelezwa kwamba siku ya tukio Kanumba alimtaka asitoke ili watoke pamoja baadae lakini ilipofika saa tano usiku alisikia vurugu chumbani kwa Kanumba ambako alikua na mpenzi wake ambae ni Lulu na baada ya muda Seth aligundua kulikua na ugomvi unaendelea na mlango ulikua umefungwa.
Maelezo hayo yameendelea kwamba baada ya muda Lulu alitoka chumbani kwa Kanumba na kumtaarifu Seth kwamba Kanumba ameanguka ambapo Seth alipoingia chumbani alikuta Kanumba kaegemea ukuta pembezoni mwa mlango huku povu likimtoka mdomoni na kuamua kumlaza chini kabla ya kuomba msaada.
Mashahidi wengine wanaotarajiwa kutoa ushahidi wao wakati kesi itakapoanza kusikilizwa ni Sophia Kassim ambae ni mmiliki wa nyumba aliyokua anaishi Kanumba, madaktari watatu, Polisi watatu, afisa uhamiaji ambae ni shemeji wake Kanumba na Moris Sekwao ambae ni kijana aliempakia Lulu kwenye gari lake muda mfupi kabla ya kukamatwa.
Baada ya kusomwa kwa maelezo ya mashahidi wote, wakili wa serikali amesoma maelezo ya Lulu na kuamplfy kwamba mwigizaji huyu alianza uhusiano wa kimapenzi na Kanumba january 2012 ambapo walikua na kutoelewana katika baadhi ya nyakati hasa pale mmoja anapompigia simu mwenzake na haipokelewi kwa wakati.
Baada ya maelezo yote kutolewa na kukamilika, Hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Augustina Mmbando amezishukuru pande zote na kumtaka Lulu atoe maelezo ya nyongeza kama anayo ambapo Lulu alisema hana maelezo yoyote ya kuongezea.
Hakimu Mmbando amemtaka Lulu kuendelea kubaki rumande mpaka tarehe ya kesi yake itakapotajwa na Mahakama kuu ya Tanzania.
Hakuna ukweli wowote wa taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Lulu ameachiwa kwa dhamana.

Thursday, November 8, 2012

HUYU NDIO MWAFRIKA TAJIRI ZAIDI BARANI AFRIKA,DUNIANI ANASHIKA NAFASI YA 62 KWA UTAJIRI

http://www.africansuccess.org/docs/image/490_Aliko-Dangote2.jpg 
Alhaj Aliko Mohamad Dangote 'ALIKO DANGOTE'

Kutokana na jarida maarufu duniani kwa kutoa takwimu za kifedha za matajiri wakubwa duniani imethibitika kuwa Aliko Dangote ambae ni raia wa Nigeria mmiliki wa makampuni ya Dangote Group ndie mwafrika anaeongoza kwa utajiri barani Afrika wakati akishika nafasi ya 62 huku utajiri wake ukikadiriwa kufikia zaidi ya $ 13.5 Bilioni. Siku za hivi karibuni bilionea huyu alitembelea Tanzania na kuanzisha kampuni ya uwekezaji wa uzalishaji wa seruji.
 
Muonekano wa Jarida la Forbes la mwezi November 2012.
Hapa akiwa na Mhe Pinda

SOMA BARUA YA BEYONCE KWA RAISI OBAMA

beyonce open letter to obama

Tuesday, October 30, 2012

KAMA HUKUONA BEHIND THE SCENES YA TANGAZO LA EBSS, NATABIRI SALMA YUSUPH KUONDOKA NA 50MILLION CASH PRIZE


 Hiyo ni behind the scene ya Tangazo la Epiq Bongo Star Search 2012
Natabiri tu jamani, kwa ufuatiliaji wangu wa Epiq Bongo Star Search 2012 naona kabisa huyu Salma Yusuf anaujua anafanya nini. Nampenda sana tangu nimuone siku ya kwanza kwenye audition za Zanzibar pale ngome kongwe. Ili kuufanya utabiri wangu utimie TUMA NENO 'EBSS09 KWENDA 15503

Monday, October 29, 2012

OFFICIAL TRAILER YA KUM KUBUM YA NIKKI WA PILI,ICHEKI HAPO CHINI

UTENGENEZAJI WA COVER YA TRACK MPYA YA DIAMOND IITWAYO "NATAKA KULEWA"

Huyo jamaa mweupe anaitwa Zungu, yuko na jamaa location wakijiandaa kushoot picha za cover hiyo.
.
.
.
.
.
 
 Raqey akiwa kwenye kazi yake kama kawaida. Huyu jamaa ni mzuri sana kwenye hayo mambo.
.
Jinsi Cover lilivyotokelezea

.

Friday, October 19, 2012

KILINUKA SANA LEO DAR ES SALAAM, IPO HAJA KUBWA YA KUTAFUTA UFUMBUZI WA HARAKA!

 
Wananchi wakitawanyika wakati wa vurugu eneo la Msimbazi, Kariakoo jijini Dar.
 
Polisi wakiimarisha ulinzi eneo la Kariakoo leo.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa leo katika maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam baada ya polisi kuzuia maandamano yaliyotaka kufanywa na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kitendo kilichopelekea mabomu ya machozi kulipuliwa na baadhi ya waumini hao kutia nguvuni na polisi.
 
Magari ya Jeshi la Wananchi Tanzania yakielekea Kariakoo kwa ajili ya kuimarisha ulinzi eneo hilo.
 
Jamaa huyu alidakwa na polisi wakati wa maandamano hayo.
 
Polisi wakiwatangazia wananchi waliokuwa eneo la Kariakoo kutawanyika mara moja wakati wa vurugu hizo.
 
Mama huyu alipoteza fahamu baada ya milipuko kadhaa kutokea eneo hilo.
 
Polisi wakiwa kazini kuzuia maandamano hayo.
 
Baadhi ya waandamanaji waliokamatwa wakati wa vurugu hizo wakiingizwa kituo cha polisi Msimbazi.

 
Magari ya Jeshi la Wananchi yakipita katika mitaa ya Kariakoo kuwataarifu wananchi kutawanyika eneo hilo.
Baada ya baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kutawanywa kwa mabomu na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia hapo awali, kwa sasa waumini hao wanajipanga kuvamia kituo cha polisi mtaa wa Msimbazi wakiwa katika makundi makundi mikononi wakiwa na mawe na wakiimba nyimbo. Awali magari ya Jeshi la Wananchi yalipita mitaa ya Kariakoo yakiwa na wanajeshi waliokuwa wakiamuru wananchi kutawanyika lakini hali inaonekana kubadilika maana kwa sasa waumini hao wanajikusanya upya kutimiza azma yao ya kuandamana mara baada ya kumaliza swala ya saa 10 katika msikiti wa Idrissa uliopo Kariakoo. Baadhi ya madai ya waumini hao ni KUKAMATWA SHEIKH PONDA, KUTOONEKANA KWA SHEIKH FARIDI WA ZANZIBAR NA KUKOJELEWA QURAN.

Friday, October 12, 2012

"BREAKING NEWS" VURUGU ZATOKEA MBAGALA KIZUIANI DAR ES SALAAM

Habari nilizozipata hivi punde zinadai vurugu kali zatokea eneo la mbagala kizuiani jijini Dar es Salaam baada ya Waislamu wenye hasira kali kutaka kuvamia na kukichoma moto kituo cha polisi katika eneo hilo endapo wasipopatiwa kijana aliedaiwa kukikojolea kitabu cha Quran takatifu. Tukio hilo la aina yake lililofanywa na kijana mdogo anaedaiwa kuwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza lilitokea baada ya mabishano kati yake na mwenzake ambapo walibashana kuwa mtu akikojolea kitabu hicho kitakatifu atapata uchizi, hatimaye dogo huyo akaamua kukiojolea kitabu hicho ili kumpinga rafiki yake huyo ambae nae sina taarifa zake za uhakika. Nitaendelea kukujuza zaidi kadiri habari zitakavyonifikia. Ushahidi wa picha hizo hapo chini kwa hisani ya GPL.






KINGINE KIZURI KUTOKA SETH BOSCO'S BLOG NA KANUMBA THE GREAT FILMS COMPANY.

Blog hii inakupatia nafasi wewe msomaji mjasiriamali ya kujitangaza na kutangaza biashara yako au huduma mbalimbali kama vile Catering Services, Nyumba zinazouzwa, magari, viwanja, pamoja na biashara za makampuni mbalimbali. Tangazo lako litapata nafasi ya kusomwa na zaidi ya watu elfu tano kila wiki wanaotembelea blog hii. Fursa hii ni kwa wafanyabiashara wa ngazi zote na kada tofauti. Pia tunatoa taarifa za vifo,harusi,sherehe mbalimbali pamoja na kupotelewa na vitu au mtu. Bei zetu ni sawa na bure, wasiliana nasi kwa E-Mail: seththepioneer@gmail.com au tupigie kwa +255715809043

"Lets STAND for Africa" Steven Kanumba

Wakati shirika la chakula duniani mapema jana lilitoa takwimu zilizoonesha kuwa bara la Afrika linafanya vizuri kupigana na njaa pamoja na upungufu wa chakula likiwa mbele ya mataifa ya bara la Asia kama India na mengineyo video hiyo hapo chini ulikua ujumbe kwa Wafrika wote uliotolewa na Steven Kanumba akisisitiza waafrika kulitetea bara lao na kulisimamia katika masuala mbalimbali ikiwemo usalama wa chakula pamoja na amani.

KAMA HUKUONA MKASI NA RAY KIGOSI ITAZAME HAPA ALIFUNGUKA PIA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA MAREHEM KANUMBA!

Wednesday, October 10, 2012

MAN OF THE PEOPLE







PICHA KATIKA MATUKIO  MBALIMBALI YA KIJAMII AMBAYO STEVEN ALIJIHUSISHA. HAPA ALIKUA KATIKA KAMPENI YA MAMA SHUJAA WA CHAKULA YA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA OXFAM AMBAPO YEYE ALIKUA BALOZI WAKE.

Monday, October 1, 2012

IPO SIKU MTALIPWA KAMA MNAVYOLIPWA KWA KUSEMA UONGO

KAMA HUKUONA HII NDIO ILIKUA CHRISTMASS YA MWISHO KWA KANUMBA

THE GREAT NA X MASS...

Mara baada ya kutoka kanisani niliandaa chakula nyumbani kwangu,nikachoma nyama ya mbuzi na kuku,nikaandaa vinywaji,basi nikawaarika ndugu na jamaa wachache tu waje nyumbani tufurahi xmass hii.Kila mtu nilihakikisha anapata kinywaji anachopenda hata wanywaji wa pombe nao walipata wanachokipenda.Maandiko yanasema tazama ilivyo vyema kwa ndugu kukaa pamoja na kufurahi.
Sebuleni kwangu ndio kulikuwa counter...ahhahah
Walikuepo wazee wa konyagi,wazee wa nyama choma ahahahh
Story za hapa na pale zilikuepo.
Kubadilishana mawazo.
The great na bbm?kha?

Watu wakafurahi nami nikafurahi maana nimekuwa busy sana mara shooting,mara safari nje ya nchi,mara safari za Startimes,mara safari za Oxfam,mara busy ofisini nakosa mda wa kujumuika hivi nyumbani,hivyo x mass hii nikaimaliza hivi.Zaidi ya yote sifa na utukufu nikamrudishia GEHOVA EBENEZER,GEHOVA ELISHADAI,GEHOVA SHAMA.......EMMANUEL(Mungu pamoja nasi)>>>>Originally posted by Steven Kanumba HAPA on December 26,2011<<<<<<<

Hivyo ndivyo ilivyosomeka katika blog yake siku ya tarehe 26 Desemba mwaka 2011. Napenda niseme tu kuwa siku zote ambazo nimeishi na kaka yangu marehemu Kanumba sikuwahi kufikiria kama ipo siku atakuja kuondoka kama alivyoondoka,tuliishi kwa furaha,amani upendo na ushirikiano wa hali ya juu sana,sikuonekana katika picha hizo ila nilikuepo na ndie niliepiga picha hizo. Najaribu tu kuwaonesha maisha yangu na Kanumba siku za karibia na kifo chake ili mpate kujua msichokua mnakifahamu. Mungu ailaaze roho yake mahala pema peponi.